Mazingira FM

WWF yakutana na wadau juu ya uhifadhi vyanzo vya maji

12 March 2024, 11:06 am

Enock Edward afisa mipango tathimin mafunzo na ufuatiliaji wa shirika la WWF Tanzania, Picha na Catherine Msafiri

Shirika la WWF limekutana na wadau na viongozi wa watumia maji mkoa wa Mara na maafisa mazingira ili kutathimini yale waliofanya ndani ya miezi 6 ya mradi wa uhifadhi wa Dakio la mto Mara.

Na catherine Msafiri

Shirika la WWF limekutana na wadau na viongozi wa watumia maji mkoa wa Mara na maafisa mazingira ili kutathimini yale waliofanya ndani ya miezi 6 ya mradi wa uhifadhi wa Dakio la mto Mara.

Akizungumza katika mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa muembeni complex Musoma kiongozi kutoka shirika la WWF Mhandisi.Christian  Chonya amesema mradi unamalengo makuu matatu yanayolenga kusaidia katika suala la uhifadhi mazingira na vyanzo vya maji.

Mhandisi, Chonya amesema mradi wa uhifadhi wa dakio la mto Mara  unalenga kuzijengea uwezo taasisi ili kuwawezesha kushiriki, kuratibu na kutekeleza usimamizi wa maji, kuboresha vyanzo vya maji , kuratibu mapendekezo ya mfumo bora wa malipo ili kuhifadhi na kuboresha vyanzo vya maji huku akibainisha lengo la jumla ni kusaidia kutatua changamoto za usalama wa maji.

Baadhi ya washiriki katika semina hiyo

Aidha Mhandisi.  Chonya amesema mradi unamanufaa mablimbali kama kurejesha maji, kuiwezesha jamii kutambua umuhimu wa vyanzo vya maji na kuhimili mabadiriko ya tabianchi.

Kwa upande wake Enock Edward afisa mipango, tathimini, mafunzo na ufatiliaji wa shirika la WWF Tanzania ameeleza jinsi mradi unavyokwenda na unavyotakiwa kutekelezwa  huku  akibainisha kuwa wao kama WWF wanaunga mkono kile kinachofanywa na jumuiya za watumia maji.