Mazingira FM

Mwenge wazindua madarasa tisa Chitengule sekondari

12 July 2023, 3:07 pm

Abdalah Shaibu Kaimkiongozi wa mbio za mwenge kitaifa 2023, picha na Thomas Masalu

Mbio za mwenge kitaifa bado zinaendelea mkoani mara leo mbio hizo zipo halmashauri ya wilaya ya Bunda ambapo miradi takribani 7 imetembelewa katika hatua za uwekaji wa jiwe la msingi na mingine kuzinduliwa.

Na Thomas Masalu

Mwenge wa uhuru 2023 umezindua vyumba vya madarasa tisa na ofisi Moja ya walimu katika shule ya secondary Chitengule halmashauri ya wilaya ya Bunda.

Mradi huo umetekelezwa kupitia fedha Kutoka serikali kuu kwa mwaka 2022/2023.

Uzinduzi umefanyika leo ukiongozwa na kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa ndugu Abdalah Shaibu Kaim.

baadhi ya madarasa yaliyozinduliwa na mbio za mwenge shule ya sekondari ya Chitengule halmashauri ya wilaya ya Bunda, picha na Thomas Masalu

Akizungumza katika mradi huo ndugu Kaim amesema serikali ya awamu ya sita imefanya kazi kubwa katika utekelezaji wa miradi ya kimaendeleo ikiwa ni pamoja na ujenzi wa vyumba vya madarasa.

Aidha ameitaka halmashauri ya wilaya ya Bunda kufanyia marekebisho kasoro ndogondogo zilizobainika katika mradi huo na apewe mrejesho wa kile kilichofanyika kupitia picha.

Mradi wa vyumba vya madarasa ni mradi wa sita katika orodha ya miradi ambayo imefikiwa na mwenge wa uhuru 2023.