Mazingira FM

Wafugaji wamchagua Mshota mwenyekiti taifa

11 April 2024, 11:23 am

Mrida Mshota, mwenyekiti wa wafugaji Tanzania. Picha na Adelinus Banenwa

Mrida Mshota ambaye ni mjumbe wa bodi ya wakurugenzi NARCO amefanikiwa kutetea nafasi yake ya uenyekiti wa wafugaji taifa katika uchaguzi uliofanyika 8 April 2024 Dodoma.

Na Adelinus Banenwa

Mrida Mshota ambaye ni mjumbe wa bodi ya wakurugenzi NARCO amefanikiwa kutetea nafasi yake ya uwenyekiti wa wafugaji taifa katika uchaguzi uliofanyika 8 April 2024 Dodoma.

Mrida alishinda kiti hicho baada ya kupata kura 375 dhidi ya mpinzani wake aliyepata kura 145.

Akizungumza na Mazingira Fm kwa njia ya simu Ndugu Mrida amesema kitendo cha kupata kura nyingi kutoka kwa wafugaji inamaanisha bado wana imani na naye.

Sauti ya Mrida Mshota

Aidha Mrida amesema kwa sasa vipaumbele vyake ni kujenga makao makuu ya chama cha wafugaji, kuiomba serikali kupima maeneo ya wafugaji na kuhakikisha kunakuwa na benki ya wafugaji ambayo kila mfugaji aliyesajiliwa atachangia na kupata fursa ya kukopa.

Sauti ya Mrida Mshota