

23 June 2025, 5:59 pm
Kwa baadhi ya jamii, wajane hulaumiwa kwa vifo vya waume zao, hutengwa kijamii, na mara nyingine hata kunyimwa urithi au mali walizochuma pamoja.
Na Adelinus Banenwa
Kila mwaka ifikapo tarehe 23 Juni, dunia huadhimisha Siku ya Wajane Duniani (International Widows Day), ikiwa ni fursa ya kuangazia changamoto, uonevu, na unyanyapaa unaowakumba wajane wengi hasa katika nchi zinazoendelea. Siku hii ilianzishwa na Shirika la Umoja wa Mataifa mwaka 2010 kwa kutambua hali ya mateso, umasikini na ukosefu wa haki za msingi kwa wajane duniani kote.
Wajane wengi duniani hupitia kipindi kigumu baada ya kufiwa na waume zao, si tu kiuchungu bali pia kijamii na kiuchumi. Kwa baadhi ya jamii, wajane hulaumiwa kwa vifo vya waume zao, hutengwa kijamii, na mara nyingine hata kunyimwa urithi au mali walizochuma pamoja. Katika baadhi ya mataifa, wajane huishi katika hali duni bila msaada wowote wa kijamii au kisheria.
Kauli mbiu “Innovation and technology for gender equality”yaani
“Ubunifu na teknolojia kwa usawa wa kijinsia.”