DC Bupilipili;. Awatunuku vyeti wadau wa maendeleo Bunda
5 June 2021, 8:53 am
Mkuu wa Wilaya ya Bunda Mh Mwl Lydia Bupilipili amewatunuku vyeti wadau wa maendeleo Wilaya ya Bunda katika kutambua mchango wao wa kuisaidia serikali kutekeleza miradi yake
Hafla hiyo imefanyika June 4, 2021 Wilayani Bunda ambapo pamoja na Mambo mengine mkuu wa Wilaya amewashukuru wadau wote wa maendeleo kwa namna wanavyojitolea kuisaidia serikali kutekeleza miradi ya maendeleo kwa wananchi
Bupilipili amesema serikali ya awamu ya Tano ya Hayati Magufili na Serikali ya awamu ya sita ya Mh Samia zinatambua mchango mkubwa wa wananchi wanaojitolea kufanikisha maendeleo ya nchi na wananchi
Pia mkuu huyo wa Wilaya amewataka wadau wote wa maendeleo Wilaya ya Bunda kuendelea kujitoa kufanya Kazi na Serikali kwa kuwa kile wanachokifanya kimeonekana na kwamba ameamua kutoa vyeti kwa wote waliojitoa kuisaidia serikali katika kutekeleza Ila ya chama Cha Mapinduzi ambacho kinaunda serikali
Miongoni mwa Wadau wa maendeleo waliotunukiwa cheti na Mkuu wa Wilaya ni pamoja Redio Mazingira fm ambapo kupitia kwa Meneja wa kituo Ally Simba Nyankinda amesema amepokea cheti hicho kwa Furaha na yeye kama msimamizi mkuu wa kituo Cha Redio Mazingira fm watahakikisha wanatimiza Majukumu yao ya kuhabarisha Umma kwa kila jambo linalotokea bila ubaguzi wowote.