Mazingira FM

Bunda; Diwani wa Nyasura aongoza wananchi unjenzi wa vyumba viwili vya Madara kwa nguvu zao

10 October 2022, 8:01 am

Wananchi wa mitaa ya Zanzibar na Nyasura B kata ya Nyasura Halmashauri ya mji wa Bunda wamejitolea katika ujenzi wa madarasa mawili shule ya msingi Kilimani kutokana na uhaba uliopo shuleni hapo.

 

Wakizungumza wakati wakichimba msingi tayari kwa kuanza ujenzi wamesema wamelazimika kufanya hivyo kutokana na upungufu uliopo.

mtendaji wa kata ya Nyasura Jonimary Atanasi amesema ujenzi nwa vyumba viwili vya madarasa na ofisi moja vinatarajia kughalimu shilingi milioni 40 huku wadau wa maendeleo kwa kushirikiana na wananchi watajenga boma kisha serikali itamalizia.

 

Kwa upande wake diwani wa kata ya Nyasura Magigi Samweli Kiboko amewaasa wananchi kuwa na moyo wa kujitolea katika suala zima la maendeleo ili kuifanya zanzibar kuwa ya tofauti.

Awali mwalimu mkuu wa shule ya msingi Kilimani Victor Amosi amesema shule hiyo ina upungufu wa madarasa 10 ukilinganisha idadi ya wanafunzi waliopo shuleni hivyo kitendo cha wananchi kuamua kujenga madarasa hayo kitapunguza mrundikano wa wanafunzi madarasani.