Mazingira FM

Idara ya elimu sekondari Bunda mji yawapongeza walimu na wanafunzi waliofanya vizuri 2022

12 November 2023, 11:54 am

Mkuu wa wilaya ya Bunda mwenye suti ya kaki akikabidhi zawadi Kwa mmoja ya walimu

Idara ya Elimu Sekondari halmashauri ya mji wa Bunda imefanya hafla ya kuwapongeza walimu na wanafunzi waliofanya vizuri katika mitihani ya Kidato cha Nne na Sita mwaka 2022.

Na Adelinus Banenwa

Idara ya Elimu Sekondari halmashauri ya mji wa Bunda imefanya hafla ya kuwapongeza walimu na wanafunzi waliofanya vizuri katika mitihani ya Kidato cha Nne na Sita mwaka 2022.

Baadhi ya walimu wakipokea zawadi katika hafla hiyo.

Mgeni rasmi katika hafla hiyo Mhe Mkuu wa Wilaya ya Bunda Dkt. Vicent Anney amewapongeza walimu na wanafunzi waliofanya vizuri na kuwaasa kutobweteka na ufaulu walioupata.

Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya amesema anatambua juhudi na jitihada za walimu na ndio maana anawapongeza kwa kazi nzuri wanayoifanya.

Baadhi ya wanafunzi katika Picha ya pamoja na meza kuu.

Aidha  Dr Naano amewahimiza wanafunzi kuendelea kusoma kwa bidii ili waweze kujenga kesho yao iliyo bora huku akiahidi kwa siku zijazo kuwa ataanda hafla nyingine ya kuwapatia motisha walimu ili waendelee kufanya vizuri zaidi.

Awali Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Bunda Emmanuel Mkongo alieleza dhana ya Serikali katika kuboresha Sekta ya Elimu ya Sekondari hasa kwa kuboresha miundombinu ya elimu kwa kuleta fedha za ujenzi wa madarasa na maabara za sayansi ambapo kwa Halmashauri ya Mji wa Bunda shule zote za Serikali zimepata miradi hiyo.