Mazingira FM

Nyumba zazingirwa na maji Nyatwali, wakazi wayakimbia makazi yao

29 April 2024, 11:09 am

Baadhi ya nyumba zilizoathirika na mafuriko tamau, Picha na Adelinus Banenwa

Baadhi ya wakazi wa Nyatwali katika mitaa ya Kariakoo na Tamau wamelazimika kuyakimbia makazi yao baada ya nyumba zao kuzingirwa na maji ya mafuriko, tahadhari ya magonjwa ya mlipuko yatolewa.

Na Adelinus Banenwa

Baadhi wakazi wa kata ya Nyatwali katika mitaa ya Kariakoo na Tamau wameyakimbia makazi yao na wengine kukwama baada ya nyumba zo kuzingirawa na maji ya mvua zinazoendelea kunyesha.

Baadhi ya viongozi wa kata ya Nyatwali akiwa na wahanga wa mafuriko waliokwama

Mwenyekiti  wa mtaa wa Tamau Asafu Elenest Owiti amesema zaidi ya kaya 35 zimeathirika na mafuriko ya maji ya mto Rubana baada ya mto huo kufurika, na maji yake kuingia kwenye makazi ya watu ambayo yamesababisha baadhi ya nyumba kuanguka na mashamba ya mazao kuzama kwenye maji.

Sauti ya Mwenyekiti  wa mtaa wa Tamau Asafu Elenest Owiti

Asafu amesema kaya 16 za mtaa wa Tamau ujaruoni hasa eneo la Uhuru park ndo wapo hatarini zaidi kwa kuwa mto Rubana umewaweka katikati hivyo ili waweze kuondoka wao na mali zao pamoja na mifugo yao wanahitaji msaada wa serikali.

Baadhi ya nyumba zilizoathirika na mafuriko tamau, Picha na Adelinus Banenwa
Baadhi ya nyumba zilizoathirika na mafuriko tamau, Picha na Adelinus Banenwa

Aidha Asafu amewataka wakazi wa Tamua hasa walioko maeneo ya mabonde waondoke na serikali ya mtaa itawapatia maeneo ya kukaa kwa muda.

Naye mwenyekiti wa mtaa wa Kariakoo Jumanne Yatema Abdallah amesema baadhi ya wakazi wa Kariakoo wameyakimbia makazi yao baada ya kuzingirawa na maji ya ziwa ambayo yameongezeka kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha.

Sauti ya mwenyekiti wa mtaa wa Kariakoo Jumanne Yatema Abdallah
Baadhi ya nyumba zilizoathirika na mafuriko Kariakoo, Picha na Adelinus Banenwa

Naye diwani wa kata ya Nyatwali Malongo Mashimo ambaye pia ni makamu mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa Bunda amesema kimsingi hali ya wakazi wa mitaa miwili ya Kariakoo na Tamau  maisha yao yapo hatarini kutokana na mafuruko na ongezeko la maji ziwa Victoria

Malongo amesema kuna hatihati ya kupata magonjwa ya milipuko maana vyoo vimejaa maji hivyo kufanya maji taka kuzagaa na wananchi wanakanyaga humo humo ambapo amesema tayari amewasiliana na mganga mkuu wa halmashauri kuona namna ya kusaidia wananchi hao

Sauti ya diwani wa kata ya Nyatwali Malongo Mashimo

Malongo ameongeza kuwa changamoto ya Nyatwali inatokana na mpango wa serikali kutaka kuwahamisha wakazi hao ambapo tayari tathmini imefanyika hivyo wananchi kutotakiwa kufanya ukarabati wowote wa  nyumba zao

Hivyo ameiomba serikali kama haijawa tayari kuwahamisha wakazi wa kata hiyo ni vema iwaruhusu kujenga makazi ya kudumu ili kuepukana na changamoto zinazowakabili.

Sauti ya diwani wa kata ya Nyatwali Malongo Mashimo
Baadhi ya nyumba zilizoathirika na mafuriko Kariakoo, Picha na Adelinus Banenwa

Naye katibu wa siasa na uenezi CCM kata ya Nyatwali Joseph Mwita Kibichi amesema maelekezo ya chama kwa viongozi wa kata na mitaa ya Nyatwali ni kuhakikisha wakazi wote waliopo kwenye maeneo yaliyoathirika na maji wanahamishwa haraka sana iwezekanavyo ili kuwanusuru wao na mali zao

Sauti ya katibu wa siasa na uenezi CCM kata ya Nyatwali Joseph Mwita Kibichi