Mazingira FM

Aweso aisitisha MUWASA kutoa huduma ya maji Tarime

2 March 2024, 6:34 pm

Waziri wa maji Mhe Jumaa Aweso ametangaza Muwasa kusitisha kutoa huduma ya kusambaza maji kwenye mji wa Tarime

Na Adelinus Banenwa

Waziri wa maji Mhe Jumaa Aweso ametangaza Muwasa kusitisha kutoa huduma ya kusambaza maji kwenye mji wa Tarime

Mhe Jumaa Aweso amechukua hatua hiyo kwenye ziara ya Mhe waziri mkuu Kassim Majaliwa leo ikiwa ni siku ya tatu katika ziara ya siku nne mkoani Mara.

Akijibu kero ya mbunge wa jimbo la Tarime mjini Michael Kembaki ambaye alimuomba waziri mkuu kuondoka na watu watu wa MUWASA kutokana na kushindwa kuwahudumia wananchi

Mhe Aweso amesema kuanzia sasa MUWASA wasimame kutoa huduma ta usambazaji maji Tarime na badala yake wizara inakwenda kufanya uratibu mzuri kuona wakazi wa Tarime wanapata huduma kama ilivyokusudiwa.