Mazingira FM

Bunda: Waliopigana vita ya Kagera watakiwa ofisi ya mshauri wa mgambo wilaya

29 November 2023, 7:08 pm

Salum Halfani Mtelela, Katibu Tawala Wilaya ya Bunda akizungumza na Mazingira Fm ofisini kwake. Picha na Edward Lucas

Edward Lucas

Askari waliopigana vita ya Kagera mwaka 1978-1979 waliopo Wilayani Bunda wametakiwa kufika katika ofisi ya Mshauri wa Mgambo Wilaya Bunda.

Taarifa hiyo imetolewa leo na Katibu Tawala Wilaya ya Bunda, Salum Halfani Mtelela mbele ya waandishi wa habari ofisini kwake kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Bunda Dr. Vincent Naano ambaye pia ni mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya.

Sauti ya Salum Halfani Mtelela