Mazingira FM

Watendaji watakiwa kukaa ofisini Nyasura

16 January 2024, 12:16 pm

Mwenyekiti wa CCM Nyasura mwenye shati la kijani na Diwani wa kata ya Nyasura

Wito umetolewa kwa watendaji wa serikali za mitaa kata ya Nyasura kukaa ofisini ili kutimiza adhma ya kuwahudumia wananchi.

Na Adelinus Banenwa

Wito umetolewa kwa watendaji wa serikali za mitaa kata ya Nyasura kukaa ofisini ili kutimiza adhma ya kuwahudumia wananchi.

Hayo yamesemwa na mwenyekiti wa CCM kata ya Nyasura katika kikao cha kupokea taarifa ya utekelezaji wa ilani kutoka kwa Mhe diwani ambapo mwenyekiti wa CCM amesema kuwa yamekuwepo malalamiko ya wananchi kutopata huduma katika ofisi za watendaji kwa kuwa muda mwingi ofisi hizo zinakuwa zimefungwa.

Amesema mara nyingi ofisi za watendaji zimeshuhudiwa kuwa na makufuli muda wote huku wananchi wakihangaika kupata huduma.

Pia mwenyekiti huyo amewata kawatendaji hao pia kubandika namba zao za simu kwenye ofisi zao ili pindi wanapopata dharula iwe rahisi wananchi kuwapata.

Mwenyekiti wa CCM Nyasura mwenye shati la kijani na Diwani wa kata ya Nyasura

Naye diwani wa kata ya Nyasura Mhe Magigi Samweli Kiboko ameagiza watendaji na mwenyeviti wa mitaa kuhakikisha ofisi zinakuwa wazi hata kama watakuwa kwenye vikao wahakikishe ofisi zinafunguliwa pindi vikao vinapoisha au wawe wanaacha mwakilishi.