Mazingira FM

Diwani Nyasura awapa nyenzo za kazi mabalozi Nyasura

16 January 2024, 11:59 am

Mabalozi na viongozi wa ccm kata wakiwa kwenye picha ya pamoja baada kupatiwa daftari kutoka kwa diwani wa kata hiyo Magigi Samwel Kiboko

Diwani wa kata ya Nyasura na mwenyekiti wa kamati ya maendeleo ya kata Mhe Magigi Samweli Kiboko ametoa madaftari 33 na kalamu kwa mabalozi wote wa CCM katika kata hiyo ikiwa ni sehemu ya kuwawezesha viongozi hao kufanya kazi yao vizuri.

Na Adelinus Banenwa

Diwani wa kata ya Nyasura na mwenyekiti wa kamati ya maendeleo ya kata Mhe Magigi Samweli Kiboko ametoa madaftari 33 na kalamu kwa mabalozi wote wa CCM katika kata hiyo ikiwa ni sehemu ya kuwawezesha viongozi hao kufanya kazi yao vizuri.

balozi wa ccm kata ya Nyasura akipokea daftari kutoka kwa diwani wa kata hiyo Magigi Samwel Kiboko

Mhe Kiboko ametoa vitendea kazi hivyo katika kiako cha kuwasilisha taarifa ya utekelezaji wa ilani katika kikao kilichowakutanisha  viongozi wa mtaa wakiwemo wenyeviti na watendaji pamoja na viongozi wa chama cha mapinduzi.

Mbali na kutoa vitendea kazi hivyo pia Mhe Kiboko amewalipia ada za uanachama mabalozi hao ikiwa ni muendelezo wa kutimiza ahadi yake aliyoitoa wakati wa kampeni  wakati wa uchaguzi 2020.

Kwa upande wake katibu mwenezi  chama cha mapinduzi kata ya Nyasura ndugu Frenki Lutonja amesema mabalozi hao kupewa daftari  kutakisaidia chama kupata taarifa na takwimu sahihi za idadi ya wanachama ngazi ya mashina.

Nao mabalozi wamemshukuru diwani wa kata ya Nyasura kwa namna ambavyo ameona umuhimu wa kuwapatia vitendea kazi maana ilikuwa ni changamoto katika kutekeleza majukuma yao.