Mazingira FM

Waandishi wa habari Mara wajengewa uwezo programu ya kitaifa ya malezi na makuzi ya mtoto

3 April 2024, 9:59 am

Charles Mashauri, Mwezeshaji wa Programu Jumuishi ya Taifa ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto mkoa wa Mara. Picha na Adelinus Banenwa

Vyombo vya Habari nchini vimetajwa kuwa nguzo muhimu katika utekelezaji wa Programu Jumuishi ya Taifa ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto ( PJT – MMMAM).

Na Adelinus Banenwa

Vyombo vya Habari nchini vimetajwa kuwa nguzo muhimu katika utekelezaji wa Programu Jumuishi ya Taifa ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto ( PJT – MMMAM).

Hayo yamebainishwa na Charles Mashauri ambaye ni Msimamizi Mkuu wa Miradi ya Maendeleo Kanisa la A.I.C.T Dayosisi ya Mara na Ukerewe ambaye pia ni Mwezeshaji wa Programu Jumuishi ya Taifa ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto mkoa wa Mara.

Baadhi ya waandishi waliohudhuria mafunzo PJT – MMMAM mkoa wa Mara. Picha ana Adelinus Banenwa

Akizungumza mara baada ya mafunzo hayo yaliyofanyika leo katika ukumbi wa ofisi za kanisa la A.I.C.T Bweri Musoma yakiwajumuisha waandishi wa habari 20 kutoka vyombo mbalimbali na maeneo mbalimbali ya mkoa wa Mara, Mashauri amesema jamii inapitia changamoto nyingi katika kujenga maadili ndani ya jamii hivyo vyombo vya habari vinanafasi kubwa katika kuijenga jamii.

Sauti ya Charles Mashauri,Mwezeshaji wa Programu Jumuishi ya Taifa ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto mkoa wa Mara

Aidha akizungumzia Programu Jumuishi ya Taifa ya Malezi, Makuzi na Maendeleo Awali ya Mtoto amesema lengo la programu ni kuwekeza kwa watoto kuanzia umri wa miaka sifuri hadi minane (0-8 yrs) ili kuhakikisha watoto hao wanakua katika ukuaji timilifu.

Sauti ya Charles Mashauri,Mwezeshaji wa Programu Jumuishi ya Taifa ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto mkoa wa Mara