Mazingira FM

Mtelela: Wakulima tumieni teknolojia kwenye kilimo

10 August 2023, 7:41 am

Balozi wa Pamba Nchini Tanzania Aggrey Mwanri mwenye shati nyeupe akiwa na Katibu tawala Wilaya ya Bunda Mhe Salumu Halfani Mtelela, Picha na Adelinus Banenwa

Wakulima kutumia teknolojia ili kukuza kilimo kama vile kujua ukubwa wa mashamba yao.

Na Adelinus Banenwa

Akifungua kikao kilichowakutanisha wataalam wa halmashauri zote mbili za wilaya ya Bunda katibu tawala wilaya ya Bunda Salumu Mtelela amewataka wakulima kutumia teknolojia ili kukuza kilimo kama vile kujua ukubwa wa mashamba yao.

Mtelela ameyasema hayo katika kikao cha balozi wa pamba nchini Tanzania Aggrey Mwanri  ambapo amefika Bunda kwa ajili ya kutoa elimu kwa wakulima namna ya kuandaa mashamba darasa.Picha na Adelinus Banenwa

Sauti ya Salumu Mtelela katibu tawala Bunda

Balozi Aggrey Mwanri amewataka wakulima wa zao la Pamba wilayani Bunda kuachana na kipimo Cha sentimeter 90 kwa 40 kwa kuwa vipimo hivyo vimepitwa na wakati.

Balozi Mwanri amesema wakulima hawapati mazao tarajiwa kwa sababu hawafuati utaratibu wa kilimo bora cha zao la pamba.

Washiriki wa kikao cha zao la pamba, Picha na Adelinus Banenwa

Amesema changamoto kubwa ni wakulima kutopanda pamba kwa  mstari kwa kufuata vipimo vya centemeter 60 kwa 30  pili ni kuchanganya zao la Pamba na mazao Mengine na suala maotea.

Akizungumzia kushuka kwa bei ya pamba nchini balozi Mwanri amesema hii imetokana na bei ya soko ya kidunia huku akiwakumbusha wakulima kuwa serikali haipangi bei ya pamba bali inaweka ukomo wa bei ili kumlinda mkulima.

Sauti ya Balozi wa Pamba Tanzania Aggrey Mwanri