Mazingira FM

Ziara ya Ridhiwani mkoani Mara yaondoka na waratibu wa TASAF

14 September 2023, 7:17 pm

Mhe Ridhiwani Kikwete Naibu Waziri Utumishi, Picha na Thomas Masalu

Mheshimiwa Ridhiwani Jakaya Kikwete ameagiza kufutwa mara moja mfumo wa ulipaji wa fedha kwa wanufaika wa TASAF kwa njia ya mitandao ya simu.

Na Thomas Masalu

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais- Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mheshimiwa Ridhiwani Jakaya Kikwete ameagiza kufutwa mara moja mfumo wa ulipaji wa fedha kwa wanufaika wa TASAF kwa njia ya mitandao ya simu na kwamba kuanzia sasa wanufaika wapewe fedha zao mkononi.

Kikwete ametoa maagizo hayo wakati akizugumza na wananchi pamoja na viongozi katika mkutano wa hadhara kata ya Mugeta wilaya ya Bunda mkoani Mara.

Sauti ya Mhe Naibu Waziri Utumishi juu ya kufutwa malipo ya TASAF kupitia mtandao.

Kikwete amesema mfumo huo umekuwa na changamoto kubwa na malalamiko yamekuwa mengi kutoka kwa wanufaika wa TASAF hivyo serikali hawezi kuendelee kuacha wananchi wake wateseke na kuona mradi huo kuwa ni adhabu kwao.

Aidha Kikwete ametoa onyo kwa mratibu wa TASAF wa halmashauri ya wilaya ya Bunda huku akisema tayari ameshawafuta kazi mratibu wa TASAF mkoa na waratibu wa TASAF wa Tarime na Musoma.

Sauti ya Mhe naibu waziri onyo kwa mratibu wa bunda