Mazingira FM

Tume kuundwa kufatilia miradi ya maji jimbo la Bunda

29 November 2023, 8:08 am

Pichani ni baadhi ya viongonzi wakikagua baadhi ya miradi ya maji Jimbo la Bunda. Picha na Thomas Masalu.

Naibu Katibu mkuu wizara ya maji Mhandisi Mwajuma Waziri ameagiza kuundwa kwa tume maalum ya kufuatilia miradi yote ya maji jimbo la Bunda ambayo inaonekana kukamilika wakati huo hakuna huduma yoyote ya maji.

Na Thomas Masalu

Naibu Katibu mkuu wizara ya maji Mhandisi Mwajuma Waziri ameagiza kuundwa kwa tume maalum ya kufuatilia miradi yote ya maji jimbo la Bunda ambayo inaonekana kukamilika wakati huo hakuna huduma yoyote ya maji.

Moja ya miradi ya Maji inayotekelezwa Jimbo la Bunda mjini. Picha na Thomas Masalu.

Mhandisi Mwajuma ametoa maagizo hayo wakati akizungumza na wakazi ya kijiji cha Mugeta na Mihingo kufatia ziara aliyoifanya ya kutembelea miradi mbalimbali ya maji ambayo serikali imewekeza fedha.

Naibu Katibu mkuu wizara ya maji Mhandisi Mwajuma Waziri.

Katika ziara hiyo Naibu katibu mkuu ameambatana na Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA), Mhandisi Clement Kivegalo ambapo amesema yaliyopita yamepita hivyo wakazi wategemee mabadiliko kupitia ziara hiyo.

Mhandisi Clement Kivegalo

Naye mbunge wa jimbo la Bunda Boniphace Getere amesema wananchi hawana uadui na serikali bali wanachotaka ni kuona miradi ina kamilika na maji yatoke.

mbunge wa jimbo la Bunda Boniphace Getere

Ziara ya Naibu Katibu Mkuu wizara ya maji imefanyika katika Kata 7 ambazo ni Hunyari, Mugeta, Mihingo, Salama, Nyamuswa na Nyamaguta.