Mazingira FM

CCM Bunda yapigilia msumari kauli ya Kinana, yatoa onyo wanaojipitisha kutaka uongozi

8 September 2023, 1:40 pm

Katibu wa siasa na uenezi chama Cha mapinduzi wilaya ya Bunda ndungu Gasper Petro Charles, Picha na Adelinus Banenwa

Chama Cha mapinduzi wilaya ya Bunda kimewaonya makada wa chama hicho walioanza kujipitisha katika mitaa, kata na majimbo kutaka nafasi za uongozi kwamba chama kitawachukulia hatua.

Na Adelinus Banenwa

Katibu wa siasa na uenezi chama Cha mapinduzi wilaya ya Bunda ndungu Gasper Petro Charles amewaonya makada wa chama hicho walioanza kujipitisha katika mitaa, kata na majimbo kutaka nafasi za uongozi kwamba chama kitawachukulia hatua.

Ndungu Gasper ametoa kauli hiyo wakati akifanya mahojiano na radio Mazingira Fm ambapo amesema ni kinyume Cha katiba, kanuni na Maadili ya chama hicho mwanachama kutangaza nia au kijipitisha Kwa nia ya kutaka uongozi katika maeneo ambayo viongozi bado wapo na wanaendelea na majukumu yao

Aidha ndungu Gasper amesema adhabu zipo mbalimbali endapo mwanachama atabainika kufanya vitendo hivyo ikiwa ni pamoja na onyo, onyo Kali, karipio, kusimamishwa uanachama na adhabu ya juu kabisa ni kufukuzwa uanachama.

Ikumbukwe kauli hii ya katibu mwenezi inakuja ikiwa ni siku Moja tangu makamu mwenyekiti bara wa chama hicho ndungu Abdulrahman Kinana atoe onyo sawa na hilo akiwa mkoani Arusha Kwa wanachama walioanza kujipitisha kutaka nafasi mbalimbali za kugombea akibainisha uchaguzi bado.