Mazingira FM
Mazingira FM
30 May 2026, 8:42 pm

Kujihusisha na uhamiaji haramu ama kufarisha au kutunza zipo adhabu za faini ambazo si chini ya shilingi milion ishirini na kifungo cha miaka 20 au vyote kwa pamoja lakini pia mali kutaifishwa.
Na Adelinus Banenwa
Wito umetolewa wananchi wilayani Bunda kuhakikisha wanashiri kikamilifu kwenye ulinzi wa nchi kwa kutoa taarifa za wahamiaji haramu ili kuendelea kuliweka taifa salaama
Hayo yamesemwa na Mrakibu wa Uhamiaji Sadikiel Jonas Mhomboje Afisa uhamiaji wilaya ya Bunda kupitia kipindi cha ufahamu wa sheria kinachorushwa kupitia radio Mazingira fm
Mhomboje amesema ikiwa mwananchi anamashaka na mtu yeyote kuhusiana na uraia au mienendo yake hana budi kutoa taarifa Idara ya uamiaji au kwenye ofisi yoyote ya serikali kuanzia kwa watendaji wa vijiji mpaka ofisi ya mkuu wa wilaya na wao kama Idara ya uamiaji watapata taarifa na kuchukua hatua.
Amewataka pia wafugaji wenye migodi pamoja na wavuvi ambao wapo na watumishi ambao hawana uhakika na uraia wa watu wao kuhakikisha wanawafikisha ofisi za uamiaji kujiridhisha.

Kwa upande wake Amina Rajab Mbegu mkaguzi msaidizi wa uamiaji wilaya ya Bunda amesema sheria zipo wazi kwa mtu yeyote mtanzania atakayekamatwa kujihusisha na uhamiaji haramu ama kufarisha au kutunza zipo adhabu za faini ambazo si chini ya shilingi milion ishirini na kifungo cha miaka 20 au vyote kwa pamoja lakini pia mali kutaifishwa kama ni nyumba au chombo cha usafiri kilichokuwa kikitumika na hii ni kwa mujibu wa sheria ya uhamiaji sura ya 54 marejeo ya mwaka 2023

Naye Salumu Juma Mashaka afisa wa uamiaji wilaya ya Bunda amesema kwa mujibu wa sheria ya uamiaji mtu yeyote hatakiwi kutoa ajira kwa raia wa nchi nyingine bila kujiridhisha na vibali vya uraia wake iwe ni ajira ya kawaida au kibarua na endapo ikibainika wote wawili watakuwa wametenda kosa na nikinyume na sheria.