Mazingira FM

Mkuu wa mkoa Aipongeza halmashauri ya Bunda DC Kasi ujenzi shule maalumu ya wasichana

21 September 2023, 9:34 am

Mkuu wa mkoa wa Mara Said Mohamed Mtanda mwenye nguo nyeusi akishiriki kwenye mradi wa ujenzi sekondari ya wasichana, Picha na Adelinus Banenwa.

Mkuu wa mkoa wa Mara Said Mohamed Mtanda ameipongeza Kasi ya ujenzi katika mradi wa shule maalumu ya wasichana ya mkoa wa Mara inayojengwa kata ya Butimba halmashauri ya wilaya ya Bunda.

Na Adelinus Banenwa

Mkuu wa mkoa wa Mara Said Mohamed Mtanda ameipongeza Kasi ya ujenzi katika mradi wa shule maalumu ya wasichana ya mkoa wa Mara inayojengwa kata ya Butimba halmashauri ya wilaya ya Bunda.

Akizungumza katika mradi huo katika ziara yake ya kutembelea miradi ndani ya wilaya ya Bunda Mhe Mtanda amewataka watendaji wa halmashauri kusimamia vyema ujenzi wa shule hiyo ili thamani ya fedha iweze kuonekana

Aidha Mhe Mtanda amewataka watumishi kujiepusha na kula fedha za Miradi inayoletwa katika maeneo yao.

Ikumbukwe kuwa ujenzi wa shule maalumu ya sekondari ya wasichana Mkoa wa Mara inajengwa kata ya Butimba halmashauri ya wilaya ya Bunda Kwa gharama ya shilingi billion 3 ambapo kitaifa zinajengwa shule 26

Mradi mwingine uliotembelewa ni ujenzi wa nyumba ya mwalimu shule ya Sekondari ya Sunsi.