Mazingira FM

Ushauri: Shughuli za vijana zisiathiri utaratibu wa Mungu katika maisha yao

21 June 2023, 10:16 am

Wito umetolewa kwa vijana kumtanguliza Mungu katika shughuli zao na kujiepusha na mambo yasiyofaa katika jamii.

Hayo yamesemwa na mwenyekiti wa vijana kanisa la FPCT neno la Neema Bade Winford  chini ya mchungaji Omoso Tukiko ikiwa ni hitimisho la wiki ya vijana iliyoanza tarehe 12 Juni na kutamatika 18 Juni 2023.

Bade amesema  ujumbe mkubwa walikuwa nao wiki nzima ni mahusiano ya kijana pasipo kuathiri utaratibu wa Mungu na kanisa , uchumi wa kijana , pia kumtanguliza Mungu katika kila hatua.

Bade Winford

Kwa upande wao vijana wamesema wamejifunza mambo mengi japo wanao muda mrefu katika kumtumikia Mungu lakini kupitia wiki ya vijana kuna jambo jipya wamejifunza.

Aidha wamesema changamoto kubwa waliyokutana nayo kwa vijana ni kutofanya kazi na badala yake kujiwekeza katika michezo ya kubahatisha, kamari, pamoja na ulevi.

VIJANA

Awali akisoma taarifa ya vijana Ester Gideon ambaye ni mkuu wa kitengo cha hamasa na habari idara ya vijana kanisani hapo amesema katika kipindi cha miezi sita idara ya vijana imefanya mambo mbalimbali ikiwepo kufanya uinjilisti , elimu kwa vijana na mazingira yake ,  kuhamasisha vijana kufanya kazi halali bila kuathiri uhusiano wao na Mungu.

Ester Gideon