Mazingira FM

Shule ya msingi Bigutu yakabiliwa na upungufu wa madarasa

12 November 2021, 5:38 pm

Wanafunzi shule ya msingi Bigutu wakishangilia baada ya Diwani Flavian Chacha kuwapelekea mipira miwili

Shule ya msingi ya Bigutu iliyopo kata ya Bunda stoo Halmashauri ya Mji wa Bunda inakabiliwa na chambamoto mbalimbali kutokana na idadi kubwa ya wanafunzi wanaosomea shuleni hapo

Akizungumza na Mazingira fm mwalimu mkuu wa shule hiyo Yohana Albert amesema shule hiyo ina jumla ya wanafunzi 1761  kati yao wavulana 859   wasichana 902 huku wakiwa na maitaji ya vyumba vya madarasa 42 na vilivyopo ni 12 tu 

Naye mwenyekiti wa kamati ya shule amesema anawashirikisha wazazi kuchangia maendeleo ya shule kwa kutoa michango lakini kutokana na idadi kubwa ya wanafunzi bado uhitaji ni mkubwa

Diwani wa kata ya Bunda stoo Flaviani Chacha akiwa mbele ya umati wa wanafunzi wa bigutu akisikiliza changamoto zao

Kwaupande wake diwani wa kata ya bunda stoo Mh Flavian chacha amesema atashirikiana na kamati za shuleo kuangalia namna ya kushughulikia changamoto hasa kwa kuamishia nguvu kwenye shule za msingi baada ya shule za sekondari kupata ufadhiri wa fedha ya mpango wa maendeleo wa kupambana na UVICO-19 hivyo amezitaka kamati za shule kuwashirikisha wazazi kuamishia nguvu za michango kwenye shule za msingi ambazo ziko na hali mbaya

Ikumbukwe kwamba shule ya msingi ya bigutu katika matokeo ya darasa la saba mwaka 2021  imeshika nafasi ya 20 kati ya shule  59 kwenye halmashauri ya mji wa bunda  huku ikishika nafasi ya 299 kimkoa kati ya shule 745 na nafasi ya 6423 kitaifa kati ya shule 11909

By Adelinus Banenwa