Mazingira FM

CWT Bahi ahadi kibao baada ya safari ya Serengeti

7 July 2023, 6:01 pm

Baadhi ya walimu na viongozi CWT kutoka Bahi Dodoma waliokwenda kutalii hifadhi ya taifa Serengeti, Picha na Adelinus Banenwa

Ni msafara wa walimu 42 kutoka halmashauri ya Bahi mkoani Dodoma kwenda kutalii katika hifadhi  ya taifa ya Serengeti baada ya Halmashauri hiyo kushika nafasi ya kumi kitaifa katika matokeo ya darasa la saba kwa mwaka 2023 ambapo safari hiyo imeratibiwa na ofisi ya chama cha walimu tanzania CWT taifa.

Na adelinus Banenwa

Mwenyekiti wa chama cha walimu Tanzania wilaya ya Bahi mkoani Dodoma mwalimu Hosea Mahagi Mapesi ameishukuru  Ofisi ya chama cha walimu Tanzania chini ya katibu mkuu wake Japheth Maganga kwa kuwaandalia walimu wa Bahi  ziara ya kwenda kutalii hifadhi ya taifa ya Serengeti.

Mwalimu Mapesi amesema ziara hiyo inatokana na halimashauri hiyo kushika nafasi ya 10 kitaifa katika matokeo ya mtihani wa kitaifa wa darasa la saba wa mwaka 2022 huku ikiwa ni halmashauri ya wilaya ya kwanza kushika nafasihiyo kitaifa ambapo nafasi za kwanza hadi tisa  zilishikwa  na halmashauri za majiji

wao kama walimu wakuu tayari wameweka mkakati wa kutoka katika nafasi ya kumi kitaifa hadi kufikia nafasi tano bora kitaifa katika matokeo ya darasa la Saba 2023.

 Aidha amesema motisha hiyo  kwa walimu wa halmashauri hiyo itaongeza chachu ya kufanya kazi kwa bidii ili katika mtihani uja waweze kufanya vizuri zaidi.

Baadhi ya viongozi wa CWT wilayani Bahi mkoani Dodoma waliyoambatana na walimu safari ya kwenda kutalii Serengeti, Picha na Adelinus Banenwa
Mwenyekiti wa chama cha walimu Tanzania wilaya ya Bahi mkoani Dodoma mwalimu Hosea Mahagi Mapesi

Kwa upande wake katibu wa chama cha walimu Tanzania wilaya ya Bahi Mwalimu Kemilembe Gregory amesema ziara hii itaongeza ushindani kwa halmashauri zingine ili ziweze kufanya vizuri katika matokeo ya mitihani ijayo pia wao kama Halmashauri ya Bahi kuongeza nguvu kwenye ufundishaji

katibu wa chama cha walimu Tanzania wilaya ya Bahi Mwalimu Kemilembe Gregory

Akizungumza kwa niaba ya walimu wakuu wote kutoka halmashauri ya wilaya ya Bahi Mwalimu Paschal Andrea ambaye ni mwalimu mkuu shule ya msingi Bahi Mission amesema baada ya kutoka katika  ziara ya Serengeti wao kama walimu wakuu tayari wameweka mkakati wa kutoka katika nafasi ya kumi kitaifa hadi kufikia nafasi tano bora kitaifa katika matokeo ya darasa la Saba 2023.

Mwalimu Paschal Andrea ambaye ni mwalimu mkuu shule ya msingi Bahi Mission

Naye mwalimu  Emmanuel John kutoaka idara ya  elimu halmashauri ya wilaya ya Bahi kwa niaba ya Afisa elimu wa halmashauri hiyo amewataka walimu kote nchini kufanya kazikwa umoja na kuwa na moyo wa  kujitoa kwa kuwa pasipo kujitoa hakuna kinachoweza kufanyika

Mwalimu  Emmanuel John kutoaka idara ya  elimu halmashauri ya wilaya ya Bahi