Mazingira FM

Madiwani Bunda walia na uvamizi wa nyani kwenye makazi

17 February 2024, 10:25 pm

tawala wilaya hiyo Salumu Mtelela, Picha na Adelinus Banenwa

Tutazungumza na tawa kutatua changamoto ya uvamizi wa nyani kwenye makzi ya watu Mhe Madiwani tupeni muda.

Na Adelinus Banenwa

Ofisi  ya mkuu wa wilaya ya Bunda kupitia kwa katibu tawala wilaya hiyo Salumu Mtelela imelihakikishia baraza la madiwani halmashauri ya mji wa Bunda  kuwa ofisi hiyo itakutana na mamlaka zinazohusika katika usimamizi wa wanyamapori ili kutatua changamoto ya uvamizi wa nyani na nguruwepori  katika makazi ya watu.

Ni katika kikao cha baraza la madiwani  halmashauri ya mji wa Bunda cha  robo ya pili  ya mwaka wa fedha 2023 na 2024 kilichoketi  Feb 14 , 2024.

Kauli hiyo ya Mtelela imekuja baada ya diwani wa kata ya Kabarimu Ndugu Muhunda Nyahimbo Manyonyoryo  kutaka kujua hali ya nyani na nguruwepori kufanya  uvamizi  kwenye makazi ya watu pamoja  na  mashamba ambayo yameshuhudiwa  katika  siku  za  hivi karibuni  hasa  katika maeneo ya kata ya Kabarimu mtaa wa Saranga na Kilima hewa, kata ya Nyamakokoto,  Balili miongoni mwa maeneo mengine.

baadhi ya madiwani waliochangia sakata la uvamizi wa nyani kwenye makazi ya watu, Picha na Adelinus Banenwa

Katika hoja zao madiwani wamedai kuwa katika maeneo mbalimbali ya mji wa Bunda na Hospitali ya Bunda DDH yamekuwa kitovu cha uvamizi wa nyani na imekuwa ni usumbufu kwa wagonjwa hasa  akina  mama  waliojifungua kuwa kwenye hatari ya kunyang’anywa  vyakula  vyao.

baadhi ya madiwani waliochangia sakata la uvamizi wa nyani kwenye makazi ya watu,