Mazingira FM

Diwani awavalisha kijani mabalozi wote CCM Bunda Stoo

24 August 2023, 11:41 pm

Katibu na Siasa na Uenezi CCM Wilaya ya Bunda, Gasper Charles mkono wa kulia akiwa na Diwani wa Bunda Stoo katika zoezi la kuwakabidhi sare za CCM mabalozi wa kata hiyo. Picha na Edward Lucas

Kupitia hafla ya kukabidhi sare kwa mabalozi wote wa CCM kata ya Bunda Stoo, CCM Wilaya ya Bunda yamwagia sifa Diwani Flavian kwa kukijenga chama na kusimamia shughuli za maendeleo katika kata hiyo

Na Edward Lucas

Katibu wa Siasa na Uenezi CCM Wilaya ya Bunda, Gasper Charles amempongeza Diwani wa kata ya Bunda Stoo, Flavian Chacha Nyamegeko kwa usimamizi wa shughuli za maendeleo ndani ya kata hiyo na juhudi za kukijenga chama.

Gasper ametoa pongezi hizo leo tarehe 24 Agosti 2023 kupitia hafla fupi iliyoandaliwa na Diwani Flavian ya kuwakabidhi sare za chama mabalozi wote wa CCM kata ya Bunda Stoo iliyofanyika ukumbi wa Village kata ya Bunda Stoo.

Gasper Charles, Katibu wa Siasa na Uenezi CCM Bunda akitoa pongezi zake kwa Diwani Flavian

Akizungumzia zoezi hilo , Mhe. Flavian amesema amewaandalia sare za chama (mashati) na vitendea kazi (madaftari na kalamu kwa ajili wa uwekaji wa kumbukumbu) mabalozi wote 58 wa kata hiyo ikiwa ni kutambua thamani na mchango na utekelezaji wa ahadi yake ili kuwawezesha viongozi hao kufanya kazi kwa ufanisi.

Diwani kata ya Bunda Stoo, Mhe. Flavian Chacha akizungumza na mabalozi wakati wa zoezi la kukabidhi sare ya Chama. Picha na Edward Lucas
Diwani kata ya Bunda Stoo, Mhe. Flavian Chacha

Nao baadhi ya mabalozi wakizungumza kwa niaba ya wengine wamepongeza Mhe Flavian na kusema kuwa jambo hilo linapaswa kuigwa na viongozi katika maeneo mengine huku wakimpongeza pia kwa kusimamia shughuli za maendeleo katika kata ya Bunda Stoo

Baadhi ya mabalozi wa CCM kata ya Bunda Stoo wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali. Picha na Edward Lucas
Maneno ya mabalozi baada ya kupokea sare ya chama na madaftari kwa ajili ya uwekaji wa kumbukumbu