Mazingira FM

Bunda: ajinyonga aacha watoto na mke

26 August 2023, 9:24 pm

Baadhi ya wakazi wa Kitaramanka wakiwa mbele ya nyumba ambayo mwenzao amejinyonga. Picha na Adelinus Banenwa

Akutwa amejinyonga nyumbani kwa wazazi wake chanzo hakijajulikana aacha mke na watoto wawili

Na Adelinus Banenwa

Kijana mmoja aliyetambulika kwa jina la Kija Hamis Machilu {29} mkazi wa Kitaramanka kata ya Sazira Bunda mjini amepoteza maisha kwa kujinyonga nyumbani kwa mama yake.

Tukio hilo limetokea 26 Augost 2023 ambapo kwa mujibu familia yake kijana huyo alilala kwake lakini asubuhi aliamka na kwenda kutekeleza kitendo hicho nyumbani kwa mama yake katika moja ya nyumba ambayo haitumiki kwa makazi.

Akizungumza na Mazingira Fm kaka wa marehemu Amos Machilu amesema ndugu yao hakuwai kusema kana ana tatizo lolote na wameshangaa kwa uamuzi aliouchukua wa kujitoa uhai aidha amesema kija ameacha watoto wawwili na mke mmoja

sauti ya kaka wa marehemu Amos Machilu
Baadhi ya wakazi wa Kitaramanka wakiwa mbele ya nyumba ambayo mwenzao amejinyonga. Picha na Adelinus Banenwa

Akizungumza na wakazi waliofika kushuhudia tuki hilo mkuu wa upelelezi kutoka jeshi la polisi Tanzania wilaya ya Bunda amewataka wananchi kuacha kuchukua maamuzi magumu ya kujitoa uhai kwa kisingizio cha maisha magumu aidha amesema kama jeshi la polisui tayari wamekamilisha taratibu zao za awali nawanaukabidhi mwili kwa ndugu kuendelea na taratibu za mazishi.

N.M.MISERYA mkuu wa upelelezi kutoka jeshi la polisi Tanzania wilaya ya Bunda

Kwa upande wao wakazi wa kitaramanka wameeleza kusikitishwa na tukio liliofanywa na kijana huyo huku wakiwataka vijana kuacha kuchukua maamuzi ambayo yatapelekea majonzi na masikitiko kwa familia

WANANCHI