Mazingira FM

Milioni 58 fedha mfuko wa Jimbo kutatua changamoto Bunda mji

21 November 2023, 8:42 pm

Mhe Robert Chacha Maboto, Mbunge jimbo la Bunda mjini

Kiasi Cha shilingi milioni 58 fedha za mfuko wa Jimbo zimepokelewa ndani ya Jimbo la Bunda Mjini.

Na Adelinus Banenwa

Kiasi Cha shilingi milioni 58 fedha za mfuko wa Jimbo zimepokelewa ndani ya Jimbo la Bunda Mjini

Hayo yamesemwa na mbunge wa Jimbo la Bunda Mjini Mhe Robert Chacha Maboto wakati akizungumza na radio Mazingira Fm mapema hii leo.

Mhe Maboto amesema fedha hizo baada ya kuingia jukumu lililopo ni wananchi wa Jimbo la Bunda  kuainisha vipaumbele vyao ili fedha hizo zitumike kutatua sehemu ya hizo changamoto.

Aidha Mhe Maboto amesema ofisi ya mbunge tayari imepokea kero nyingi kutoka maeneo mbali mbali katika kata 14 zinazounda Jimbo la Bunda mjini ambapo pia hizo zitaangaliwa ili kuona kama sehemu ya fedha hiyo itatumika.

Ikumbukwe kwamba fedha kama hiyo shilingi milioni 58 ya mfuko wa Jimbo ilitolewa mwaka Jana ambapo ndani ya Jimbo la Bunda Mjini Mhe Mbunge Robert Chacha Maboto alitengeneza madawati 1049 yaliyokwenda kupunguza changamoto ya upungufu wa madawati katika shule za msingi kwenye Jimbo lake.