Mazingira FM

Bunda ; Serikali ya awamu ya sita imedhamiria kuboresha miundombinu ya elimu.

28 November 2022, 10:22 pm

Naibu waziri wa TAMISEMI mh. David Silinde amesema kuwa serikali ya awamu ya 6 inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassani imedhamiria  kuboresha miundombinu ya elimu shule ya msingi  na ekondari ili wanafunzi waweze kufurahia mazingira ya Shule.

Ametoa taarifa hiyo wakati wa ziara yake ya kikazi  wilaya ya Bunda alipotembelea shule ya sekondari ya Bunda kugagua ujenzi wa vyumba wa madarasa unaoendelea shuleni hapo.

Mhe Shilinde  amfenya ziara Nov 27 na kukagua ujenzi wa vyumba vya madarasa shule ya sekondari bunda pamoja na shule ya Sekondari Nyamakokoto zinazopatika halmashaui ya mji wa Bunda.