Mazingira FM

Auawa kwa kisu kisa 1000 ya kamali

29 September 2021, 10:22 am

Ni Jumanne Jackson miaka 21 mkazi wa mtaa wa kabusule Kata ya Nyamakokoto Halmashauri ya Mji wa Bunda amechomwa kisu nakupoteza Maisha katika ugomvi wa kamali

Tukio hilo limetokea September 28, 2021 majira ya jioni ambapo kwa kujibu wa mashuhuda wa tukio hilo wamesema walisikia ugomvi katika chumba alichokuwa akiishi Marehemu na baada ya kutoka nje walimuona mtuhumiwa akikimbia huku Marehemu akiwa ameinama huku damu zikichuruzika chini.

moja ya ndugu wa Marehemu huyo alisema “nilisikia mlango unagonga puuuuh sikustuka maana hii milango inatumia nguvu kuifungua Ila sijakaa vizuri nikaitwa bibi bibi wanagombana huku nilipotoka nje nikakuta wanasukumana huyu kijana aliyefariki na kijana aliyekuwa anagombana naye akiwa ameshika kisu kikiwa na damu walitoka nje Jumanne aliinama Chini huku damu zikiwa zinamtoka gafla akachomwa kisu kingine kisha mtuhumiwa akikimbia”

Kamanda wa jeshi la police mkoa wa Mara Longinus Tibishubwamu amethibitisha kutoka kwa tukio hilo na kusema kuwa sababu ya ni ugomvi wa kamali ambapo Marehemu alishinda sh. 1000 jambo ambalo mtuhumiwa hakukubaliana nalo na kuamua kumshambulia kwa kisu na kusababisha kifo chake

Aidha kamanda Tibishubwamu amesema mtuhumiwa anashikiliwa kituo Cha Polisi Bunda na mwili wa Marehemu umehifadhiwa Hospitali ya DDH Bunda

Kamanda Tibishubwamu ametoa wito kwa jamii kuvumiliana na kuwa na utu ili kuacha matendo mabaya

By Adelinus Banenwa