Mazingira FM

Wakulima wahimizwa kulima kitaalamu

27 May 2026, 10:48 am

Baadhi ya wakulima skimu ya Kisangwa

Kutokea skimu ya kisangwa jumla la wakulima 214 wamenufika kutoka vijiji vya Kiroreli, Nyangere na kijiji cha Kambubu.

Na Adelinus Banenwa

Wito umetolewa kwa wakulima kuzingatia taratibu za kilimo ili kuweza kuongeza mavuno na kipato cha familia.

Hayo yameelezwa na Fabiola Ranga mratibu uhailishaji wa teknolojia na mahusiano TARI Dakawa ambapo amesema kilichoonekana kwa wakulima ilikuwa ni ukosefu wa elimu ambapo wakulima walikuwa wakitumia mbegu za kienyeji hivyo kushindwa kupata mavuno ya kutosha.

Aidha Fabiola amesema TARI Dakawa wamewaletea wakulima aina tano za mbegu zenye tabia tofauti kutokana na mazingira ambapo wakulima watachagua kulingana ba matokeo ya mavuno katika eneo hilo.

Sauti ya Fabiola Ranga

Benson Nturi afisa kilimo halmashauri ya wilaya ya Bunda amesema kutokea skimu hiyo ya kisangwa jumla la wakulima 214 wamenufika kutoka vijiji vya Kiroreli, Nyangere na kijiji cha Kambubu.

Amesema changamoto kubwa iliyokuwepo kwa wakulima ni ukosefu wa elimu kwa kuwa walikuwa wakitumia mbegu za asili pia walikuwa wakilima bila kufuata utaratibu wa kilimo bora hasa upandaji upaliliaji na utunzaji wa mashamba.

Sauti ya Benson Nturi

Tatu Masunga moja ya wakulima katika skimu ya Kisangwa amesema kwa miaka miwili ambayo amekuwa mkulima katika skimu hiyo ameona mafanikio makubwa huku akiwashukuru TARI kwa kuwaletea mbegu bora ambazo zitawasaidi kupata mavuno mengi

Amesema mwanzo walikuwa wakivuna gunia 10 lakini baada ya kupata elimu ya kilimo bora kwa sasa wanavuna gunia 30 hadi 40 kwa ekari 1.

Amesema moja ya faida alizozipa ni pamoja na kumlipia ada mtoto wake hadi kumaliza chuo kikuu lakini pia amefanikiwa kununua mifugo ( ng’ombe)

Sauti ya Tatu Masunga