Mazingira FM

Km 25 barabara za lami kupendezesha mitaa Bunda

2 July 2023, 3:43 pm

Mkuu wa wilaya ya Bunda Dk Vicent Naano amesema serikali imeleta fedha kwa ajili ya ujenzi wa barabara kilometa 25 za lami ndani ya barabara za mitaa Bunda mjini,  stendi mpya ya kisasa, soko, pamoja na machinjio.

Dc Naano ameyasema hayo katika mkutano wa hadhara alioufanya kata ya Kabarimu alipofika kuzungumza na wananchi na kusikiliza kero zao.

Dk Vicent Naano

Aidha amewataka wafanyabiashara wa mbao, uchomeleaji, watengenezaji wa fenicha kujiandaa kwa kuwa watalazimika kuondoka katikati ya mji ili kurahisisha mji kupangwa vizuri.

Dk Vicent Naano

Katika ziara hiyo mkuu wa wilaya aliongozana na viongozi kutoka taasisi zote za umma ikiwa ni pamoja na BUWSSA, TASAF, TANROAD, KILIMO na MIFUGO miongoni mwa taasisi zingine.

Katika hatua nyingine DC Naano amewataka wataalam kutoka halmashauri na taasisi za serikali kushughulikia changamoto za wananchi ili kuepusha migogoro.