Mazingira FM

Bunda; Mahakama ya wahukumu faini ya laki tatu au kifungo cha miaka mitatu jela watu wawili kwa kosa la kukutwa na mali ya wizi

2 December 2022, 12:26 pm

Mahakama ya wilaya ya Bunda mkoani Mara imewahukumu kulipa faini ya shilingi laki tatu au kwenda jela miaka mitatu Mwenge Maseke (29) mkazi wa bunda mjini na Guya Saimon Isabuke (41) mkazi wa Bunda stoo (ambaye hakuwepo mahakamani) kwa kosa la kukutwa na mali ya wizi

Hukumu hiyo imetolewa leo tarehe 1 Dec 2022 na Hakimu Mkazi Mfawidhi Mwandamizi wa mahakama hiyo Mhe. Mulokozi Paschal Kamuntu.
Awali imedaiwa mahakamani hapo na mwendesha mashtaka Tryphone Makosa Jacob Mkaguzi Msaidizi wa polisi amesema mnamo tarehe 22 mwezi wa 12 mwaka 2021 majira ya usiku katika eneo la Saranga kwenye mnara wa Vodacom uliopo mtaa wa Saranga Bunda mjini watuhumiwa hao wanadaiwa kuvunja na kuiba betri tatu za mnara huo aina ya HTT France Limited zenye Thamani ya shilingi Milion mbili laki tano na hamsini na tisa elfu .

Mhe. Kamuntu amesema baada ya kusikiliza pande zote mahakama imejiridhisha pasipo shaka kwamba katika makosa waliyoshtakiwa nayo watuhumiwa ya kuvunja na kuiba mahakama imewakuta hawana kosa.
Kamuntu ameongeza kuwa kwa mujibu wa kifungu cha 306 cha sheria ya muenendo wa makosa ya jinai sura ya 20 mahakama imewakuta na kosa mbadala la kukutwa na mali ya wizi kinyume cha kifungu cha 311 cha sheria kanuni ya adhabu sura 16.
Kutokana na kosa hilo mahakama imewahukumu kulipa faini ya shilingi laki tatu au kwenda jela miaka mitatu na kulipa fidia ya shilingi million mbili huku akiamuru pikipiki yenye namba za usajili T 318 BFJ iliyotumiwa kusafirisha mali ya wizi kuuzwa kwenye mnada wa adhara na pesa itakayopatikana itumiwe na serikali.