Mazingira FM

Ujumbe wa WWF kwa wadau wa Uhifadhi

15 September 2023, 1:32 pm

Mratibu wa Programu za Maji Baridi WWF Tanzania, Eng.Christian Chonya

Na Edward Lucas

Wadau wametakiwa kuwa na Ushirikiano ili kufanikisha juhudi na mikakati yote ya uhifadhi wa Bonde la Mto Mara kwa ajili ya uhifadhi endelevu.

Wito huo umetolewa na Mratibu wa Programu za Maji Baridi kutoka WWF Tanzania, Eng. Christian Chonya wakati akizungumza na Radio Mazingira baada ya kushiriki katika Kongamano la Kisayansi Jumuiya ya Afrika Mashariki ya Bonde la Ziwa Victoria katika Ukumbi wa Kisare Mugumu Serengeti.

Eng. Chonya amesema ili kufanikisha mikakati yote inayowekwa na wadau mbalimbali katika Uhifadhi wa mto Mara, wadau wanatakiwa kuwa na Ushirikiano.

Sauti ya Eng. Christian Joseph Chonya

Akizungumzia Kongamano hilo amesema kwa Upande wa WWF wamewasilisha mambo mawili ikiwa ni pamoja na kuelimisha kuhusu umuhimu wa kanuni bora za kugawana maji pamoja na namna bora ya kuongeza thamani katika magugu maji ili kuyatokomeza.

Maadhimisho ya 12 ya Siku ya Mto Mara yanafikia tamati Leo huku mgeni rasmi akitarajiwa Naibu Waziri wa Maji, Eng. Maryprisca Mahundi