Mazingira FM

Radio Jamii zanolewa juu ya umuhimu kutumia mitandao kuhabarisha umma

4 July 2023, 11:24 am

Waandishi wa habari na viongozi wa vituo vya Radio Jamii wakifuatilia somo kwa umakini, Picha na Mrisho Sadick

Katika kuziimarisha Radio za Kijamii, Tadio imetoa mafunzo kwa waandishi wa habari namna ya kuchapisha habari katika mtandao na faida zake katika ulimwengu wa kidigitali.

Na Ally Nyamkinda

Radio za Kijamii zimepewa mafunzo ya namna ya kuzipa nguvu habari katika maeneo yao na kutumia mitandao ya kijamii kwa manufaa katika kusambaza habari.

watu wengi wanatamani kusikia au kupata habari kutoka katika maeneo yao

Akizungumzia mafunzo hayo Mkufunzi kutoka TADIO, Amua Rushita amesema watu wengi wanatamani kusikia au kupata habari kutoka katika maeneo yao hivyo katika mafunzo hayo wameanza kwa kuwajengea uwezo waandishi kuandika habari, kuzipa kipaumbele na kutumia picha na sauti ili kuziongezea nguvu habari zao.Mkufunzi wa mafunzo kutoka Tadio Amua Rushita

mkufunzi wa mafunzo kutoka tadio Amua Rushita