Mazingira FM

Bunda: Tembo aua mmoja ajeruhi mmoja

6 September 2021, 4:43 pm

By Adelinus Banenwa

Kwandu Mtorogo (67) mkazi wa mtaa wa butakare kata ya bunda stoo wilayani bunda amepoteza maisha kwa kukanyagwa na tembo wakati anatoka kusenya kuni

Tukio hilo limetokea leo sept 5, 2021 ambapo kwa mujibu wa mashuuda wamesema mama huyo alishindwa kukimbia kutokana na umri wake pia tembo walikuwa na hasira

Kwa upande wake afisa wanyamapori wa halmashauri ya mji wa bunda ndugu hassani mkande amesema wananchi ni muhimu kuchukua tahadhari muda wote kwa kuwa tembo kwa kipindi hiki wamekuwa wengi na saa nyingine wanakuwa wamechokozwa

Naye diwani wa kata ya bunda stoo flavian chacha amesema ni wakati sasa serikali kujali wananchi kwa kuwa kimekuwa kilio kila wakati kwa tembo kusababisha madhara kwa wananchi ila hakuna hatua zinazochukuliwa kunusulu maisha na mazao ya wananchi

Naye mbunge wa jimbo la Bunda mjini Mh Robert Chacha Mabotto amesema ameisha zungumza na waziri wa maliasili na amehaidi kutembelea maeneo yote yanayopakana na hifadhi ya Serengeti ili kujionea hali ya madhira yanayowapata wananchi kutokana na wanyama Waharibifu Wakiwemo Tembo

pia amewataadharisha wananchi wote wa jimbo la Bunda Mjini kuchukua taadhari dhidi ya wanyama hao kwa kuwa ni wengi na shida hii siyo Bunda tu.