Mazingira FM

BUWASSA watakiwa kutatua changamoto ya maji chuo cha ualimu Bunda

19 April 2024, 12:34 pm

Baadhi ya viongozi waliohudhuria mahafali ya 38 chuo cha ualimu Bunda, Picha na Theresia Thomas

Mwenyekiti wa CCM Bunda aitaka BUWASSA kutatua changamoto ya maji chuo cha ualimu Bunda.

Na Theresia Thomas

Wito umetolewa kwa mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira Bunda BUWSSA  kutatua changamoto ya upungufu wa maji safi chuo cha ualimu Bunda.

Wito huo umetolewa na mgeni rasmi Leonard Magwayega mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi chama cha mapinduzi CCM  katika mahafali ya 38  ya chuo cha ulimu Bunda yaliyofanyika leo tarehe 18 April 2024 katika ukumbi wa chuo hicho.

Baadhi ya viongozi waliohudhuria mahafali ya 38 chuo cha ualimu Bunda, Picha na Theresia Thomas

Magwayega amesema changamoto ya upungufu wa maji katika chuo hicho haitakiwi kukaa muda mrefu pasipo kupatiwa ufumbuzi.

Sauti ya Leonard Magwayega, Mgeni rasmi mahafali ya chuo cha ualimu Bunda

Katika hatua nyingine Magwayega amewataka wahitimu kuitendea haki elimu walioipata.

Kwa upande wake mkuu wa chuo hicho Mwl Venance Mwita Mancheye amewataka wahitimu hao kujiajiri na kujitole sehemu zinazotoa huduma ya elimu ili kupata ujuzi, sifa na uzoefu wa taaluma waliyonayo.

Sauti ya Mwl Venance Mwita Mancheye mkuu wa chuo cha ualimu Bunda

Aidha ameishukuru serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa  kuendelea kuwezesha mazingira rafiki ya chuo na kuhudumia stahiki za watumishi wa chuo pamoja na wanachuo.

Baadhi ya wahitimu wa mafunzo ya ualimu katika mahafali ya 38 chuo cha ualimu Bunda, Picha na Theresia Thomas

Awali akisoma risala ya wahitimu ngazi ya Stashahada na Astashahada mbele ya mgeni rasmi Kija Elias, amesema  upungufu wa huduma ya maji katika chuo hicho imekua ikileta usumbufu kwa wanachuo hao.

Sauti ya Kija Elias, muhitimu wa chuo cha ualimu akisoma risala

Jumla ya wahitimu kwa ngazi ya Astashahada na Stashahada ni 369, wasichana wakiwa 166 na wavulana wakiwa 203.