Mazingira FM

DC Naano aipa kongole halmashauri ya Bunda Mji usimamizi wa miradi

6 September 2023, 12:37 pm

Dkt Vicent Naano,DC Bunda aliyesimama akizungumza kwenye baraza la madiwani Halmashauri ya mji wa Bunda, Picha na Adelinus Banenwa

Mkuu wa wilaya ya Bunda Dkt Vincent Anney Naano ameipongeza halmashauri ya mji wa Bunda Kwa usimamizi mzuri wa miradi ya Maendeleo inayoletwa halmashauri ya nji wa Bunda

Na Adelinus Banenwa

Mkuu wa wilaya ya Bunda Dkt Vincent Anney Naano ameipongeza halmashauri ya mji wa Bunda Kwa usimamizi mzuri wa miradi ya Maendeleo inayoletwa halmashauri ya nji wa Bunda

Dkt Naano ameyasema hayo katika kikao Cha baraza la madiwani halmashauri ya mji wa Bunda katika kikao Cha robo ya nne ya mwaka 2022 na 2023 yaani April na June.

DC Naano amesema halmashauri ya mji wa Bunda imejitahidi kusimamia suala la miradi japo zipo changamoto ndogondogo lakini wakifanya kazi Kwa ushirikiano hasa idara ya ujenzi mambo yatakwenda vizuri.
Ameongeza kuwa yale maelekezo yaliyotolewa katika ziara ya kamati ya siasa ya chama Cha mapinduzi katika marekebisho katika baadhi ya miradi ameona yameanza kufanyiwa kazi akitolea mfano shule ya msingi Mazoezi.

sauti ya mkuu wa wilaya ya Bunda Dkt Vincent Anney Naano

Katika hatua nyingine mkuu wa wilaya amenyooshea kidole kamati ya manunuzi kwenye miradi akitaja kununua vitu tofauti na bei ya soko akitolea mfano kamati Moja iliyonunua mbao ya 2 by 2 Kwa shilingi 8500 wakati bei ya kawaida ni shilingi elfu 4000.

sauti ya mkuu wa wilaya ya Bunda Dkt Vincent Anney Naano