Mazingira FM

Aneth Nyamuziga achangia mbao 50 ujenzi nyumba ya katibu UWT Bunda

12 March 2024, 1:48 pm

Mjumbe wa  mkutano mkuu UWT,  CCM taifa na  mjumbe wa halmashauri kuu CCM wilaya ya Ngara Aneth Philemon Nyamziga mwenye kipaza sauti akizungumza kwenye maadhimisho ya siku ya mwanamke duniani kwa wilaya ya Bunda, Picha na Adelinus Banenwa

Mjumbe wa  mkutano mkuu UWT,  CCM taifa na  mjumbe wa halmashauri kuu CCM wilaya ya Ngara Aneth Philemon Nyamziga  amewapongeza wanawake wa CCM wilaya ya Bunda kwa kujitoa kukijenga chama na jumuiya ya wanawake bila kuchoka.

Na Adelinus Banenwa

Aneth aliyasema hayo katika maadhimisho ya siku ya wanawake duniani ambapo kwa upande wa UWT Bunda maadhimisho hayo yalifanyika March 7, 2024 mjini Bunda ambapo Aneth alifika kama mgeni mwalikwa,

Mjumbe wa  mkutano mkuu UWT,  CCM taifa na  mjumbe wa halmashauri kuu CCM wilaya ya Ngara Aneth Philemon Nyamziga mwenye kipaza sauti akizungumza kwenye maadhimisho ya siku ya mwanamke duniani kwa wilaya ya Bunda, Picha na Adelinus Banenwa

Anethi alisema kaulimbiu ya mwaka huu ya siku ya mwanamke duniani iwe chachu katika kuleta mabadiliko kwa mwanamke mwenyewe katika suala la kujikwamua kiuchumi, kiuongozi na kijamii kwa ustawi wa taifa na ustawi wa jamii  kwa ujumla.

Mbali na wito huo kwa wanawake pia Aneth alichangia mbao 50 kwa ajili ya kuezekea nyumba ya katibu wa UWT Bunda ambapo kupitia maadhimisho hayo yaliyoambatana na harambee ya uchangiaji vifaa vya kumalizia ujenzi wa nyumba ya katibu wa UWT  Bunda.