Mazingira FM

Bunda: wakazi wa mcharo walia na ukosefu wa maji Safi huku miradi ikiwa imesimama muda mrefu

24 August 2022, 8:27 pm

Wakazi wa Mcharo halmashauri ya mji wa Bunda waendelea kulia na changamoto ya upatikanaji wa maji huku wakipoteza matumaini ya kukamilika kwa mradi wa maji katika eneo hilo ambao ulianza kuweka matumaini makubwa.

 

Wakizungumza na Radio Mazingira Fm iliyofika eneo hilo katika kuangalia changamoto ya upatikanaji wa maji, wakazi hao wamesema mpaka sasa wanaendelea kutumia maji kutoka katika vyanzo visivyokuwa na uhakika.

Zawadi James ni mkazi wa eneo hilo amesema wanalazimika kutembea mwendo mrefu kubeba ndoo ya maji kichwani au kununua maji kwa gharama ya shilingi 200 hadi 500 kwa ndoo

 

Lucia Masanja ambaye pia ni mjumbe wa serikali ya mtaa amesema tangu kuanza mpango wa ujenzi wa mradi wa maji katika eneo hilo uliibua matumaini makubwa lakini ni muda mrefu sasa hawaoni chochote kinachoendelea na mradi huo ukiwa umesimama.