Mazingira FM

Bunda; 4 Sept 2021 siku ya usafi wilaya nzima

2 September 2021, 7:55 pm

By Hawa Mbulula

Salum Mtelela katibu tawala wilaya ya Bunda :PICHA NA THOMAS MASALU

Katibu tawala wa wilaya ya bunda Salum Mtelela ametoa wito kwa wananchi wote wa bunda kwa ujumla kuwa tarehe 4/9/2021 siku ya jumamosi ni siku ya usafi  mkoa wa mara

Mteela ameyasema hayo leo sept 2 ,2021 katika ofisi za wilaya  kwa niaba ya mkuu wa wilaya  mtelela amesema kuwa wananchi wote wanatakiwa kufanya usafi bila kujali jinsia wala itikadi za vyama vyao

Charles Waitara mwenyekiti wa machinga mkoa wa Mara :PICHA NA ADELINUS BANENWA

Kwa upande wake mwenyekiti wa wajasiriamali mkoa wa mara Charles Waitara amesema kuwa mazingira bado ni machafu pia ameiomba serikali itoe gari ili isaidie shughuli za usafi