Mazingira FM

Bunda: Nyamakokoto yapiga marufuku wenye nyumba kupangisha bila barua ya utambulisho

15 June 2023, 11:21 am

Diwani wa kata ya Nyamakokoto Halmashauri ya Mji wa Bunda Mhe EMANUEL MALIBWA  amepiga  marufuku kwa wenye nyumba kuwapangisha watu bila  kuwa na uthibitisho wa barua alikotoka.

Akizungumza katika kikako cha  hadhara  mtaa wa barabara ya Ukerewe halmashauri ya Mji wa Bunda katika mwendelezo wa ziara yake  amesema matukio ya wizi yaliyoshamiri katika kata hiyo yanachangiwa na wenye nyumba kupangisha watu wasio waaminifu na wasiyofahamika walikotoka.

Amesema kuanzia sasa  mwenye nyumba yeyote atayepangisha mpangaji chumba bila taarifa watafikishwa polisi yeye na mpangaji wake.

Emmanuel Malibwa

Aidha Mh. Malibwa amesema uongozi wa kata utaanzisha oparesheni maalum ya kusaka na kutawanya vijiwe vyote vya bangi ambavyo ndivyo vinavyochochea uhalifu katika kata hiyo huku akiliomba jeshi la polisi kuwachukulia hatua kali watakaofikishwa kwao kwa makosa ya kujihusisha na masuala ya bangi.

Emmanuel Malibwa

Kwa upande wake D/Sgt  Athuman Salimu kwa niaba ya mkuu wa kituo cha polisi Bunda amewataka wananchi kushirikiana na jeshi la polisi katika masuala ya ulinzi kwa kuwa jukumu la ulinzi ni la kila mtanzania kwa mujibu wa sheria

Hata hivyo amewataka wakazi wa Nyamakokoto kufuata utaratibu wakati wa kutoa taarifa za matukio ya kihalifu ili kuweza kupata msaada wa haraka.

D/Sgt  ATHUMAN SALIMU