Mazingira FM

Siku ya hedhi duniani, huduma kwa mtoto wa kike zipoje?

28 May 2025, 6:52 pm

Wanafunzi shule ya sekondari Bunda mjini wakiwa na mwalimu wao mlezi wakiwa wameshikilia taulo za kike siku ya hedhi duniani

Siku ya Hedhi Duniani ambayo huadhimishwa kila mwaka tarehe 28 Mei, ni jukwaa la kimataifa linalotumika kuongeza uelewa kuhusu hedhi kama hali ya kawaida ya kibaiolojia.

Na Adelinus Banenwa

Lengo kuu la maadhimisho haya ni kuondoa unyanyapaa unaozunguka hedhi, kuhamasisha upatikanaji wa huduma salama na vifaa vya kujihifadhi, pamoja na kushinikiza usawa wa kijinsia.

Chumba maalumu na kichomea taka vilivyojengwa shule ya sekondari Bunda mjini kwa lengo la kuweka mazingira wezeshi kwa mtoto wa kike anapoingia kwenye siku zake akiwa shuleni

Katika makala hii, tutazungumzia umuhimu wa elimu ya hedhi kwa watoto wa kike hasa waliopo shuleni, mafanikio yaliyopatikana katika ngazi ya jamii na serikali za mitaa, pamoja na changamoto ambazo bado zinahitaji suluhisho la pamoja ambapo kauli mbiu ya mwaka huu inasema – Wezesha mazingira ya hedhi salama yenye utu kwa wasichana na wanawake wote.

makala