Mazingira FM

Chomete aipongeza CCM, serikali utatuzi changamoto za wananchi Bunda

30 November 2023, 6:27 pm

Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Mara kupitia CCM Ghati Chomete, akizungumza na wakazi wa Kung’ombe katika mkutano wa hadhara. Picha na Adelinus Banenwa

Mbunge wa viti maalum Ghati Chomete  amepongeza jitihada za serikali na viongozi wote wilayani Bunda kwa jitihada wanazozionesha katika kutatua changamoto za wananchi.

Na Adelinus Banenwa

Mbunge wa viti maalumu mkoa wa Mara kupitia Ghati Chomete  amepongeza jitihada za serikali na viongozi wote wilayani Bunda wa chama cha mapinduzi na wale wa serikali kwa jitihada wanazozionesha katika kutatua changamoto za wananchi.

Mbunge wa viti maalumu mkoa wa Mara kupitia Ghati Chomete katikati akiwa na viongozi wengine wa CCM Bunda kwenye ofisi za chama wilaya ya Bunda, Picha na Adelinus Banenwa.

Mhe mbunge ameyasema hayo Nov 29 , 2023 alipofanya ziara yake ya kikazi wilayani Bunda katika jimbo la Bunda Mjini na kufanya mkutano wa hadhara eneo la Kung’ombe  kata ya Kabasa.

viti na meza vilivyoletwa na Mhe Mbunge Ghati kwenye zahanati ya Kung’ombe, Picha na Adelinus Banenwa.

Katika ziara hiyo pia Mhe mbunge ametoa viti vinne na meza mbili vya kisasa  kwenye   zahanati  ya Kung’ombe ili kusaidia huduma ya afya iwahi kuanza  hasa ukizingatia uhitaji wa huduma katika  eneo  hilo.

Mbunge wa viti maalumu mkoa wa Mara kupitia Ghati Chomete, akikabidhi mtungi wa gesi kwa moja ya mwakirishi wa kikundi, Picha na Adelinus Banenwa.

Aidha mbunge Ghati ametoa majiko ya gesi kwa vikundi  10 vya akinamama wajasiriamali yanayolenga kuwasaidia wanawake kuachana na matumizi ya mkaa na kuni .

Mbunge wa viti maalumu mkoa wa Mara kupitia Ghati Chomete, akiwa na maafisa usafirishaji, Picha na Adelinus Banenwa.

Katika hatua nyingine mbunge  Ghati ametoa vizibao (refractor) kwa maafisa usafirishaji maarufu (bodaboda) zenye  lengo la kupungu za ajali za barabarani.

Aidha amemuelekeza mganga mkuu wa Halmashauri ya Bunda Mjini  kuhakikisha anatatua changamoto walizotaja wananchi hasa za akinamama kuombwa fedha wakati wanapotaka kujifungua katika vituo vya kutolea huduma za afya.