Mazingira FM

Mtoto wa miaka 14 ashikwa na mamba akiogelea ufukwe ziwa Victoria Bunda

22 December 2023, 8:26 am

Mtoto aliyetambulika kwa jina la Nyambega Elisha Mbayi mwenye umri wa miaka 14 mwanafunzi wa darasa la saba shule ya msingi Bulamba ameshikwa na mamba wakati akiogelea katika mwalo wa kitongoji cha Mwaloni.

Akizungumzia tukio hilo Afisa tarafa wa tarafa ya Kenkobyo Boniphas Maiga amesema tukio hilo limetokea jioni ya 21 Desemba 2023 wakati mtoto huyo akiogelea na wenzake huku akibainisha kuwa jitihada za kumtafuta zinaendelea.

Aidha Maiga amewataka wananchi wanaoishi kandokando ya ziwa kuchukua tahadhari ya kwenda kwenye fukwe ili kuepukana na matukio ya kushikwa na mamba.