Mazingira FM

Kilele cha wiki ya sheria nchini, Bunda ukatili kwa watoto bado upo

1 February 2024, 7:56 pm

Mkuu wa wilaya ya Bunda Dkt Vicent Aney Naano, Picha na Adelinus Banenwa

Mkuu wa wilaya ya Bunda Dkt Vicent Aney Naano amevitaka vyombo vinavyosimamia sheria kuhakikisha haki inatendeka hasa katika kesi zinazohusu ukatili wa kijinsia.

Na Adelinus Banenwa

Mkuu wa wilaya ya Bunda Dkt Vicent Aney Naano amevitaka vyombo vinavyosimamia sheria kuhakikisha haki inatendeka hasa katika kesi zinazohusu ukatili wa kijinsia.

Dc Naano ameyasema hayo katika kilele cha wiki ya sheria ambapo kwa wilaya ya Bunda sherehe hizo zimefanyika katika viwanja vya mahakama ya wilaya ya Bunda

Baadhi ya viongozi wilayani Bunda katika kilele cha wiki ya sheria nchini, Picha na Adelinus Banenwa

Mhe mkuu  wa wilaya amesema yapo mashauri mengi ya ukatili yanaonekana kuwa na changamoto kutokana na baadhi ya idara za ustawi wa jamii na madawati ya jinsia kutofuatilia mashauri hayo kwa kina

Paschal Mulokozi Kamuntu Hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama ya wilaya ya Bunda, Picha na Adelinus Banenwa

Kwa upande wake Paschal Mulokozi Kamuntu Hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama ya wilaya ya Bunda amesema taasisi ya mahakama kama mdau wa karibu wa sheria wametekeleza mambo mbalimbali katika kipindi chote cha wiki ya sheria.

Aidha Kamuntu amesema kuwa mahakama imeanzisha program ambazo zinawezesha mtu kufungua na kuendesha kesi hata bila kuwe mahakamani pia ambayo inajulikana kama mahakama mtandao