Mazingira FM

Mtelela: Viongozi fanyeni ziara na mikutano kutatua kero za wananchi

17 February 2024, 10:42 pm

Katibu tawala wilaya ya Bunda Salumu Mtelela, Picha na Adelinus Banenwa

Katibu tawala wilaya ya Bunda amewaelekeza madiwani  chini ya mwenyekiti wa halmashauri na wataalam wa halmashauri wilaya ya Bunda chini ya mkurugenzi mtendaji kufanya ziara na mikutano ya hadhara ili kusikiliza na kutatua kero za wananchi.

Na Adelinus Banenwa.

Katibu tawala wilaya ya Bunda Salumu Mtelela amewaelekeza madiwani  chini ya mwenyekiti wa halmashauri na wataalamu wa halmashauri wilaya ya Bunda chini ya mkurugenzi mtendaji kufanya ziara na mikutano ya hadhara ili kusikiliza na kutatua kero za wananchi.

baadhi ya watumishia Bunda Dc, Picha na Adelinus Banenwa

Akizungumza katika baraza la madiwani kikao cha robo ya pili ya mwaka wa fedha 2023 na 2024 Mtelela amesema imekiwa ni jambo la kusikitisha sana kuona umati mkubwa wa wananchi wakija kila siku za alhamisi kwenye ofisi ya mkuu wa wilaya na kero ambazo zingine zingetatuliwa ngazi za vijiji ama vitongoji au zingine ngazi za kata.

mkurugenzi mtendaji halmashauri ya wilaya ya Bunda Bi Changwa Mkwazu, Picha na Adelinus Banenwa

Kwa upande wake mkurugenzi mtendaji halmashauri ya wilaya ya Bunda Bi Changwa Mkwazu amesema tayari idara ya Utumishi ndani ya halmashauri hiyo wameanza ziara hizo za kutatua na kusikiliza kero na maelekezo ya katibu tawala lazima yatekelezwe.

Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Bunda Mhe Charles Magafu Manumbu, Picha na Adelinus Banenwa

Naye mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Bunda Mhe Charles Magafu Manumbu amesema maelekezo kwa madiwani kusikiliza na kutatua kero katika maeneo yao yalishatolewa muda mrefu na mkuu wa wilaya ambapo utaratibu unawataka kila siku za jumanne wawepo kwenye ofisi za kata, na kwa msisitizo alioutoa katibu tawala lazima wafanye jitihada za utekelezaji.