Mazingira FM

Aliyekuwa diwani wa Kisorya kuzikwa jumatatu kwa mujibu wa familia

15 March 2024, 4:54 pm

Marehemu Lufunjo Mafuru Ndaro, diwani wa Kisorya enzi za uhai wake, Picha kutoka maktaba

Aliyekuwa diwani wa Kisorya kuzikwa jumatatu kwa mujibu wa familia familia yasema alikuwa haumwi yasubiri majibu ya uchunguzi.

Na Adelinus Banenwa

Mafuru Phinias Mafuru kijana wa marehemu ameiambia Mazingira Fm kuwa kama familia wamesikitishwa na tukio la kuondokewa na mzazi wao huku akibainisha kuwa kilikuwa ni kifo cha gafla maana alikuwa haoneshi dalili zozote za kuumwa.

Mafuru amesema kuwa awali alikuawa anaumwa lakini lilikuwa jambo la muda mrefu na alikuwa anahudhuria kila mwezi kliniki hospitali ya Kamanga iliyoko jijini Mwanza na kwa maelezo ya daktari alisema anaendelea vizuri.

Mafuru ameongeza kuwa kama familia wanasubiri vipimo vya uchunguzi wa madaktari ndo vitaonesha chanzo cha kifo cha mzazi wao.

Marehemu Diwani Lufunjo Mafuru Ndaro amezaliwa mwaka 1957 na amefariki 2024 hivyo amefariki akiwa na umri wa miaka 67.