Mazingira FM

Kisangwa yafanya maafali ya 31 Maji yawa kero chuoni hapo

28 November 2021, 7:50 am

Wanafunzi wapatao 126 level ya pili kutoka chuo Cha maendeleo ya Wananchi Kisangwa FDC wanategemea kumaliza masomo yao mapema mwezi huu

wahitimu wa fani Mbalimbali chuoni Kisangwa FDC

Akizungumza katika maafari mkuu wa chuo Cha maendeleo ya Wananchi Kisangwa Edmund Nzowa amesema maafari hayo ni ya 31 tangu chuo hicho kianzishwe lakini changamoto kubwa ya Maji

Aidha Nzowa amesema chuo Cha Kisangwa kilikuwa na idadi ndogo ya wanafunzi Ila kwa sasa kuna takribani wanafunzi wa mafunzo ya Muda mrefu 288 huku huku kozi ya Muda mfupi iliyofadhiriwa na ofisi ya waziri mkuu ikiwa na wanafunzi 140 ambayo unafanya jumla ya wanafunzi chuo Cha Kisangwa kuwa 428

Mgeni Rasmi Afisa Elimu ya watu wazima wa Halmashauri ya Mji wa Bunda Samwel Maiga Kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Bunda amesema kwa sasa serikali imewwkeza kwa kiasi kikubwa kwenye vyuo vya wananchi lengo likiwa ni kuwaendeleza vijana katika fani Mbalimbali pia kupambana na ukosefu wa ajira

Maiga ameongeza kuwa serikali imeandaa Mpango wakuwarudisha shuleni wanafunzi walioacha shule za msingi na sekondari kwa sababu mbalimbali hasa wanafunzi wa kike waliopata ujauzito
Ambapo watatumia vyuo hivyo vya maendeleo ya Wananchi kuwajengea uwezo katika fani watakazozichagua pamoja na kuwasaidia kusoma masomo waliyoyakosa katika mfumo rasmi wa elimu

By Adelinus Banenwa