Mazingira FM

Kambarage atoa mabati 50 ujenzi nyumba ya katibu UWT Bunda

8 March 2024, 10:40 am

Mwenyekiti wa kamati ya fedha na uchumi CCM wilaya ya Bunda Eng Kambarage Wasira, Picha ana Adelinus Banenwa

Mwenyekiti wa kamati ya fedha na uchumi CCM wilaya ya Bunda Eng Kambarage Wasira ametoa mabati 50 ujenzi nyumba ya katibu UWT Bunda

Na Adelinus Banenwa

Mwenyekiti wa kamati ya fedha na uchumi CCM wilaya ya Bunda Eng Kambarage Wasira ametoa mabati hamsini katika jitihada za kuunga mkono wanawake kuelekea kilele cha siku ya mwamke duniani katika ujenzi wa nyumba ya katibu wa UWT Bunda.

kamati ya utekelezaji UWT Bunda wakifurahia kupokea mabati 50 kutoka kwa Eng Kambarage

Kambarage amesema msukumo wa falsafa ya kumuwezesha mwanamke kiuchumi katika kuharakisha maendeleo ni msingi katika mabadiliko katika sekta mbalimbali za uzalishaji ambapo amesema kwa sasa haipingiki kuwa wanawake wamepiga hatua kubwa kwenye maendeleo.