Mazingira FM

Waliofukiwa na kifusi mgodi wa Kinyambwiga Bunda mmoja apatikana akiwa amefariki

27 December 2023, 1:20 pm

Kamanda wa zimamoto na uokoaji Mkoa wa Mara Mrakibu wa polisi Agostino Magere

Mwili wa mchimbaji mmoja umepatikana baada ya taarifa ya kufukiwa na kifusi wiki mbili zilizopita katika mgodi wa Kinyambwiga wilayani Bunda mkoani Mara

Na Adelinus Banenwa

Mwili wa mchimbaji mmoja umepatikana baada ya taarifa ya kufukiwa na kifusi wiki mbili zilizopita katika mgodi wa Kinyambwiga wilayani Bunda mkoani Mara.

Akizungumza na Mazingira Fm Kamanda wa zimamoto na uokoaji Mkoa wa Mara Mrakibu wa polisi Agostino Magere amesema mwili huo umepatika Jana majira ya mchana na tayari mtu huyo ametambulika Kwa jina la Michael Mlechi (25) Pia mwili umekabidhiwa Kwa ndugu Kwa ajili ya kuendelea na taratibu za mazishi.

Aidha amesema Bado kikosi hicho Kwa kushirikiana na wachimbaji wanaendelea na jitihada za kutafuta mchimbaji mwingine Kwa kuwa taarifa zilitaja walikuwa wachimbaji wawili waliofukiwa na kifusi siku ya tukio.

Ikumbukwe taarifa za wachimbaji haoa wawili wa madini katika mgodi wa kinyambwiga zilitolewa mwanzoni mwa mwezi dec ambapo jitihada zikiendelea kufanyika hali mbaya ya mazingira ya uokoaji ikitajwa kama sababu ya kuchelewesha zoezi hilo.