Mazingira FM

Mbunge Maboto akerwa na wizi wa taa za barabarani Bunda

1 February 2024, 3:22 pm

Atakayetoa taarifa au kumkamata mwizi wa taa za barabarani kupewa donge nono.

Na Adelinus Banenwa

Atakayetoa taarifa au kumkamata mwizi wa taa za barabarani kupewa donge nono.

Ni kauli ya Mhe Robert Maboto Mbunge wa Jimbo la Bunda Mjini wakati akizungumza na wananchi na viongonzi kata ya Kabarimu eneo la Maralinti Bunda Mjini.

Mhe Maboto ameeleza kusikitishwa kwake baada ya kupewa taarifa taa za barabarani king’olewa na watu wenye nia ovu ambapo jumla ya taa mbili zimengolewa karibu na shule ya Sekondari ya Nyiendo.

Mhe Mbunge amewataka wananchi kuwa walinzi wa miundombinu ya barabara Kwa kuwa serikali inatumika gharama kubwa katika ujenzi wake.

Aidha ameahidi kutoa donge nono kwa mtu yeyote atakayefanisha kumkamata mtu anayehusika na wizi na uharibifu huo.

Kwa upande wake Meneja TANROARD mkoa wa Mara amesema kuhujumu miundombinu ya barabara ni kinyume na sheria huku akibainisha kuwa hata vibao vya alama za barabarani navyo vinang’olewa kwenye barabara mpya ya Kisorya – Nyamuswa.

Meneja huyo amesema jukumu la kuilinda miundombinu hiyo ni la kila mwananchi.